Friday, July 6, 2012

UJUMBE MUHIMU

Habari za leo mwanajumiya mwenzangu,kama unataka kutaarifiwa kwa E-mail wakati kunakuwa na post au maoni katika blog yetu basi njia ni rahisi sana. hapo kulia kwako utaona mahali pameandikwa FOLLOW BY E MAIL:andika E-mail address yako hapo na kisha fuata maelekezo kadri unavyoendelea na ukishamaliza hapo utakuwa unapata taarifa kama kuna lolote jipya katika blog yetu.
Ninawatakia wakati mzuri na weekend njema
Dr J Kingo

                                       

Friday, April 20, 2012

WIKI YA MISUKO SUKO

Wiki hii tunayoimaliza leo haikuwa ya furaha kwa wanajumuiya kwani imetuacha na misiba miwili ya wanajumuiya wenzetu Christina Mwapule na Frida leo walioondokewa na dada zao Felista mwapule na Hilder Leo.Ingawa kupoteza mmoja kati ya tunaowapenda na kuwafahamu ni majonzi makubwa lakini pia matukio haya yanatukumbusha ahadi ya Mwenyezi Mungu kuwa sisi ni MAVUMBI na mavumbini tutarudi.Kwa kukumbuka ahadi hii basi tunahitajika kuyatenda yaliyo mema kwa kadri ya uwezo wetu ili  siku yetu ikifika tuache kumbu kumbu ya mema na si kuacha mjadala wa "aaaa ni afadhali amekwenda huyu".Kwa niaba ya wanajumuiya wa jimbo la ughaibuni ninatoa salamu za rambi rambi kwa familia ya Christina mwapule na Frida Leo kwa kuondokewa na wapendwa dada zetu.Mungu awape nguvu na azipokee roho za marehemu hawa mahali pema peponi.


Mungu ametoa na Mungu ametwaa jina lake litukuzwe.


AMINA

Saturday, March 17, 2012

sekiidar@yahoogroups.com

Kujiunga na yahoo mailing group kwa wana Sekii Dar weka email address yako, submit na subiri approval toka kwa moderator
Subscribe to sekiidar

Powered by us.groups.yahoo.com

Monday, March 12, 2012

WARAKA WA WAZI KWA WANAJUMUIYA ASAA

Ninapenda kutanguliza salamu za wiki mpya ya mwezi wa tatu katika mwaka mpya nikiamini kuwa wengi wetu kama si wote tuko salama na tunaendelea na shughuli zetu kama ambavyo Maanani ametujalia.Ninaomba kwenda haraka sana kwenye hoja muhimu ili nisiwachose kusoma,kuna msemo usemao maji na mafuta huwa hayachanganyikani kwa namna yeyote,hii ikiwa na maana uovu na uadilifu pia havina nafasi huria katika chombo kimoja.Ninaandika waraka huu kwa masikitiko kwa sababu moja kati ya maji au mafuta imetaka kuingia mahali ambapo si muafaka,wala si kwa wakati bali kwa hashiria tata,ninaomba kuwakumbusha wajumbe wenzangu wale mlionitakungilia au niliowatangulia kuliona jua na kwa uchungu zaidi"kuona lango kuu"la shule ambayo leo imetufanya watoto wa baba na mama mmoja ARUSHA SEKONDARY.nina uhakika kila mmoja wetu anafahamu kuwa hakuingia langoni kwa makosa bali kwa sababu alipaswa kuwa pale,kuna marafiki,ndugu jamaa,kaka,dada,baba,mama,wake,waume,wapenzi na wengi ambao bado ni wapendwa wetu na hawakuwa na bahati ya kuingia lango lile.Nimepokea kwa mshituko mpasuko wa jitihada za kutufanya tuwe tofauti, na chanzo chake ni katika jimbo kuu la Arusha.Kwa kawaida ndimi zikishikwa na kifafa huwa haziteti na pambano gumu ulingoni likikolea basi ushindani huwa mtafaruku.Kwa sasa jungu kuu limeingia mafuta ya taa na pilau hailiki tena ati kwa sababu ya usemi usemao sisimizi kuuwa tembo!!!! lakini je kwani chawa hasumbui mwenye gwanda?sasa kama sisimizi amejaribu kuua tembo je tuna uhakika gani kuwa huenda huyu wa sasa si sisimizi bali chawa tu au kunguni ambaye dawa yake tunaifahamu!!! kuacha uchafu,kulinda mazingira ila si kwa Tembo ambaye lazima maji ayanywe!.wajumbe wenzangu kwa kweli kama tunafahamu kwanini tumekubali kuwa pamoja katika jumuiya hii,tunakubali kuyumbishwa na sauti moja ya pepo mchafu!! tena tukasahau kabisa kuwa hata sisi tuna nafasi ya kuwa na maamuzi kama watu wazima!! tukasusia vikao vya maana na kukumbatia majungu,bila kukumbuka tunadhamira ya kuona kuwa tunasonga mbele!!!tumekubali kupokonywa chembe ndogo ya msimamo na kiumbe ambaye siamini kama ni binadamu kamili lahh ni shetani katika muono mpya!!!!tumekubali atuingilie na kutufanya kama makarukenya!!! na bado tumempa hatamu huku tukishangilia kuwa ooohhh sekiii ni ya majungu na umbea tuuuuuu!!!!.Ni nani kati yetu ambaye ni sekii kama si sisi wote na mmoja wetu akitupotosha kwa wendawazimu wake tukamfuata basi sisi ni wendawazimu kuliko yeye!!!.Ninawaomba nikiwasihi,wale wote mliokwazwa na mpotoshaji huyu mjiangalie upya na mkumbuke nafasi yenu katika jumuiya"mkole kuwa mtumbwi si ajabu,mwembe hauzai dafu na mvuvi havuliki.ya dunia ni mengi na kuishi kwingi ni kuona mengi.tukumbuke akili ni nywele na kila mtu ana zake,kidole kimoja hakivunji chawa.ninaandika waraka huu nikiwaomba samahani kwa minaji iliyowasibu,tukumbuke ya kwetu na tushikilie kilicho chetu,majahazi yanapasuka sembuse siye mitumbwi!!!!wajumbe wote mliotaka kujiengua rudieni jamvini tusimulie hadithi na tukumbuke kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi.nawatakia wakati mwema na mema yote ya maanani.
Dr Joseph R Kingo a.k.a Nuhu Salehe Kilua(mtumishi wenu jimbo la ughaibuni)

Sunday, March 11, 2012

Salaam wana sekii. Jana 10/03/2012 wanajumuiya wa sekii Dar walikutana rose garden, na tunafurahi kuona kuwa jumuiya yetu inaendelea kukua, baada ya kupata wanajumuiya kadhaa wa darasa la 92 ambao wamekuwa wakikutana kwa utaratibu wao kwa muda sasa as the class of 92, na walipojua kuwa kuna sekii alumni wameona ni wazo zuri na wameridhia kuwa sehemu ya hiyo jamii, na pia walikuwepo wengine wa clas of 94, 96, na 98 ambao pia ilikuwa ni mara yao ya kwanza kufika.
Katibu wa Sekii Dar anaweka sawa yaliyojiri hiyo jana, na baadae tutayabandika hapa ubaoni.
Sekii....
Pamoja.
Pamoja?
Tunaweza.

 Hapa ni baadhi ya waliofika, wakimsikiliza Daudi Matle aliyesimama

 Kisaka Mavoa (94) aliyesimama na Esther Robert Mattle (96) aliyeka.

  Kisaka Mavoa (94) aliyesimama na Esther Robert Mattle (96) aliyeka.

 Cheggy Mziray (94) na Daudi Matle (92)

 Cheggy Mziray (94) na Daudi Matle (92)

 Toka kushoto Martin Mbotto, Daudi Mavura, Nancy Sayore, Vumilia Kaaya, Laban Kisali (Jacob Laban Kisali) hawa ni class of 94





 Ritha Alex, Atupele Mwakalinga na Jonas Joseph class of 96

 Widimi (95), Prosper Mosha (98), Ritha (96),na Atupele (96)




 Atupele, Jonas na Samuel class of 96



 Daudi, Ms Shuma, na Zubeda class of 92

 Jacob Laban, Esther Robert na Daudi Matle

































Irene Walala (96), Martin Mbotto (94), Daudi Mavura (94), na Nancy Sayore (94)










Tuduma katika umoja wetu.

Tuesday, February 7, 2012

TAARIFA KUHUSIANA NA KATIBA

                                                KATIBA
- Baadhi ya wajumbe waliomba muda wa kujadili Katiba uongezwe ili watu wazidi kutoa maoni yao, lakini kutokana na kikao cha tarehe 26/01/2012 ilionekana kuwa tukiendelea kusubiri watu wajadili hatutakaa tuikamilishe mapema,hivyo iliamuliwa kuwa Katiba ikabidhiwe kwa Muheshimiwa Judith Lohay atuunganishie zote mbili pamoja na kuileta kwetu ili tuipitie na kuchagua lugha ipi itumike.Hivyo basi tumeondoa ukurasa wa kutoa maoni kuhusiana na katiba ila tutaipandisha katiba na kuanza rasmi mchakato rasmi wa lugha itakayotumiwa na katiba yetu kama ilivyoelezwa hapo juu.
Ninawatakia kazi,afya na muda mzuri katika kuendeleza jumuiya yetu.
Asanteni sana.

Dr Joseph Kingo.
(mwenyekiti Ughaibuni)

Tuesday, December 20, 2011

Jumuiya ya wana sekii walikutana Jumapili 18/12/2011 jijini Dar na majimbo ya ughaibuni, jimbo kuu Arusha na wenyeji Dar kama inavyoonekana katika picha waliwakilishwa. Mengi yamezungumzwa. Tusubiri majumuisho ya yale yaliyozungumzwa kupata  mwanga na kuchangia maoni yetu.
sekii...
Pamoja.
Pamoja?
Tunaweza.





Martin Mbotto, Samuel Mponezya
Peter Mathias, Linnus Chalamila, Hebert Hatibu, William Joshua
Daudi Mavura, Hebert Hatibu, William Joshua, Kisaka Mavoa,