KIKAO CHA TANO CHA ARUSHA SEKII ALUMNI (ASAA) KILICHOFANYIKA AICC CLUB TAREHE 25/02/2012
Kikao kilifunguliwa saa 11:15 jioni.
1. WALIOHUDHURIA
a. Evelyn Amani
b. Anna Mushi
c. Hellen Kasegenya
d. Gilda Sangawe
e. Julius Makara
f. Alex Kiondo
g. William Joshua
2. WASIOFIKA
Hatukupata taarifa zozote kutoka kwa wajumbe walioshindwa kufika.
3. AGENDA MPYA
3.1 UKARABATI WA MAABARA YA KIFARANSA
Mwenyekiti aliona tuwaachie uongozi wa shule pamoja na Moses waendelee na swala la kukarabati darasa hilo maana tulipotaka kusaidia Moses pamoja na Mkuu wa Shule tumeshindwa kuwaelewa kwa kutuacha njia panda. Kabla ya tarehe 20/02/2012 tulienda shuleni pale ilituone kama mafundi walishaanza kazi lakini tulikuta hakuna kinachoendelea hivyo tukaomba mjumbe mmoja afike tarehe 20/02/2012 kuangalia kama kuna maendeleo yoyote lakini alikuta mafundi hawajaanza kazi. Hivyo tumeona tulikuwa tunakimbizwa mchakamchaka bure tumeona swala hili tuwaachie kina Moses waendelee wenyewe sisi tuendelee na mpango wetu wa mwanzo wa kupaka shule rangi na kutengeneza madirisha.
3.2 SWALA LA KUMSUPPORT MJUMBE MWENZETU JULIET KICHAO
Mwenyekiti alishaongea na Mwenyekiti wa Dar na kumueleza kuhusu kumsupport mwenzetu ambaye anauguliwa na Baba yake Mzazi, tuliombwa wana umoja wote tuchangie fedha kuanzia sh.10,000/= na tujitahidi kumfikishia Mweka Hazina tarehe 03/03/2012. Tunaweza kumtumia Mweka Hazina wetu pesa hizo kwa njia ya MPESA namba ya Mweka Hazina (Hellen Kasegenya) ni 0754 288768.
Kikao kijacho tutakutana tarehe 10/03/2012, saa tisa kamili mchana sehemu AICC Club.
Kikao kilifungwa saa kumi na mbili na robo jioni.
Evelyn Amani(Katibu)
Jimbo kuu la Arusha.