Kamati ya Uchumi na Mipango
Ripoti ya kwenda kuona uongozi wa Shule tarehe 27/01/2012.
Walioudhuria:-
1. Anna Mushi
2. Evelyn Amani
3. Evans Shirima
4. Julius Makara
Tuliweza kufika Shuleni saa nne asubuhi na kuonana na Mkuu wa Shule Msaidizi (Mwl Swedi) na kumweleza lengo letu la kufika pale. Alituomba tumuone Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ( Mr. Shakir ), ambapo tulienda na kufarijika sana kwa maelezo aliyotupatia.
Kwa kuwa yeye ni mjenzi ilikuwa rahisi sana kwake kutuahidi kuwa atakamilisha survey yake na kututumia quotation ndani ya siku mbili. Tulimuomba agawe majengo katika block nne (4), ili tuone wapi tunaweza kuanza napo kutokana na fedha tutakazokuwa nazo.
Tulifurahi kusikia binti yake alimaliza pia shuleni hapo. Naye aliweza kutoa mchango mkubwa wa kiasi cha Tsh. Milioni 7 kuongezea katika ukarabati wa Hostel ya wasichana na vyoo vya Waalimu.
Tulipata muda pia wa kuelezewa matatizo yaliyopo hapo shuleni mengine ambayo Julius Makara ataweza kusaidia yaweze kutatuliwa mapema iwezekanavyo.
Tunasubiri quotation tutatumiwa kwenye email, tukiipata tu tutawajulisha mara moja.
Evelyn. A.
Katibu.