Tuesday, December 20, 2011

Jumuiya ya wana sekii walikutana Jumapili 18/12/2011 jijini Dar na majimbo ya ughaibuni, jimbo kuu Arusha na wenyeji Dar kama inavyoonekana katika picha waliwakilishwa. Mengi yamezungumzwa. Tusubiri majumuisho ya yale yaliyozungumzwa kupata  mwanga na kuchangia maoni yetu.
sekii...
Pamoja.
Pamoja?
Tunaweza.





Martin Mbotto, Samuel Mponezya
Peter Mathias, Linnus Chalamila, Hebert Hatibu, William Joshua
Daudi Mavura, Hebert Hatibu, William Joshua, Kisaka Mavoa,

Wenyeviti wetu (Dar, Arusha na Ughaibuni)

Sunday, December 11, 2011

MUUNGANIKO WA WANASEKII

Kutokana na ucheleweshaji wa michango na...
Emma Mrosso 12:40am Dec 12
Kutokana na ucheleweshaji wa michango na kutoshirikiana ipasavyo sherehe ya reunion imeonekana iwe Jan. 2012 kwasababu wajumbe wenzetu
( mwenyekiti )DR JOSEPH, na mweka hazina ALOYCE MBULLU SUSA) wote ni wa jimbo la ughaibuni watakuwepo kipindi hicho hivyo ni vyema taratibu zetu ziendelee kama awali TZS 20,000 kwa kila mjumbe. Asanteni sana tunawatakia kila la kheri katika sikikuu za Noeli na Mwaka mpya.

Miss
Emma Mrosso
Katibu, Jimbo kuu Arusha Sekii, Arusha

Saturday, December 10, 2011

UTEUZI WA KATIBU WA JIMBO LA UGHAIBUNI

napenda kuwataarifu rasmi wanajumuiya wenzangu kuwa katibu mpya wa jimbo letu la ughaibuni ni bi YASMIN DOLLY uteuzi wake unaanza mara moja kuanzia leo 11/12/2011 hii ni kutokana na kujivua madaraka kwa katibu wa awali(Mr Jackob Mlagala).ninaomba ushirikiano wenu kwake kwa niaba ya wanajumuiya wa sekii jimbo la ughaibuni.Mungu awape salama.Dr Joseph R.Kingo
mwenyekiti  jimbo la ughaibuni.

Sunday, November 27, 2011

MAONI KUHUSIANA NA KATIBA

Natumai wajumbe wezangu tuko salama,kabisa na pilika zetu za maisha ya kila siku,nimeweka kivuli cha katiba iliyoandaliwa na tume iliyoteuliwa kutoka Jimbo la Dar.unaweza kuipitia ukifuata ukurasa(page)ambayo inaonekana upande wa kulia kwako inayosomeka kama ifuatavyo.KATIBA YETU TOA MAONI.
naomba tutoe maoni ili kuboresha katiba hii na michango ya kukubaliana au kutofautiana nayo ili tuweze kufanya marekebisho na hatimaye tuwe na katiba rasmi.HII NI COPY TU YA KATIBA NA WALA SI KATIBA RASMI.ninawatakia tena wakati mwema na maandalizi mazuri ya siku kuu za Noel na Mwaka mpya.

Dr Joseph.Kingo

Thursday, November 24, 2011

KATIBA

Ninapenda kuwakumbusha wajumbe wenzangu kuwa chanzo cha kupooza kwa hari iliyokuwapo mwanzo kuhusiana na jumuiya yetu unatokana(kwa maoni yangu) na kucheleweshwa pasipo sababu za msingi na mchakato wa katiba ambayo ndiyo mwongozo mama wa shughuli zetu,hivyo wanajumuiya wanachoka kusikiliza na kusoma mambo yasiyo ya msingi na  yanayopoteza muda mwingi sana na kutia maudhi,na badala yake kuhamia kwenye mambo mengine ambayo yanaonekana ni ya maana zaidi kwa maisha kuliko malumbano.Nina imani kabisa kama tutaanza upya kushughulikia katiba basi tutakuwa na mwamko na Ari ya kuchangia au hata kutokea kwenye vikao vyetu kama ilivyokuwa awali.basi ninatoa changamoto kwa majimbo mufti yanayoshughulikia swala la katiba kutupa mwanga wa wapi tumefikia na ni nini tunatakiwa kufanya ili tuwe na kitu cha kujadili kwa sababu bila ya kufanya hivyo tutabaki kuongea ni nani alimaliza mwaka gani na ni nani alipata alama gani kisha tutavuna kuchukiana na kubebeshana lawama pasipo kufahamu.Ninawatakia wakati mwema na shughuli njema hasa kwa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.
Dr J Kingo
mwenyekiti jimbo la ughaibuni

Wednesday, November 23, 2011

REUNION;REUNION

hello,

Kwa wale watakaopendelea kushiriki reunion party munataarifiwa kuwakilisha michango yenu mapema kwa mweka hazina Hellen Kasegenya au katibu Emma Mrosso. Ni kiasi cha shs 20,000. Pia kwa wale wenye wasiwasi wa fedha zao kuTumika visivyo napenda kuwataarifu shughuli nzima ya reunion ni yetu wote, tutapangilia fedha zetu wote na kuamua tufanyie nn na kitakacho bakia tutaamua kwa pamoja fedha zifanyie nn.


Pia reunion haikuweza kufanyika km ilivyokua imepangwa kwani fedha zilizopatikana zilikua hazitoshei.


Naona mwanzo tulianza na nguvu nyingi Ambazo sikudhania Ingefikia kua na ukimya kiasi hiki, bado sijachoka kuwahamasisha na ninaamini Pamoja tunaweza.


Miss Emma
Katibu Jimbo kuu la Arusha

Wednesday, October 5, 2011

WANAJUMUIYA TUMEPATWA NA MSIBA

 
 
Mwenzetu Anna Denis Mushi,
 
amefiwa na baba yake usiku wa kuamkia 02/10/2011, Msiba unafanyika Fire [nyumba za national milling] Arusha. Mazishi yatafanyika nyumbani kwao URU - Moshi siku ya Alhamisi.Baba ataagwa Mt Meru Hospital Kesho [Alhamisi] 06/10/2011 saa mbili asubuhi.Kwa wale watakao penda kushiriki katika mazishi URU - MOSHI kutakua na mabasi Yatakayo anza safari hapo mt meru hospital, nauli ya kwenda na kurudi itakua TZS 7,000.
tafadhali mwenye rambi rambi anaweza kuwakilisha kupitia kwa Emma Mroso au kwa Hellen Kasssegenya.
Mungu ailaze roho ya marehemu baba yetu mahali pema peponi.

Anna Mushi anapatikana kwenye namba +255 752136713

Thursday, September 29, 2011

KIKAO CHA TATU JIMBO KUU LA ARUSHA 25/09/2011 OLDUVAI INN ARUSHA




TAARIFA YA KIKAO CHA WANAJUMUIYA WA ARUSHA SEKII JIMBO KUU LA ARUSHA 25/09/2011 OLDUVAI INN ARUSHA



MAHUDHURIO
William Joshua
Hellen Kasegenya
Emma Mrosso
Evelyne Amani
Julieth Kichao
Anna Denis
Mariam Mgonja
Senorina John
Kazeni Amini

UDHURU
Godwin Sangawe – Mwenyekiti Msaidizi
Wilfred Kadege
Shufaa Kaduni
Evans Shirima
Nazira Kassou
Gilda Sangawe
Jackline Masao
Amina Rajabu


                                                         AGENDA


A. KATIBA
Arusha sekii ni muungano wa hiari wa 
1.   LENGO
Kuwaunganisha kwa pamoja watu wote waliosoma Arusha Sekii na kujadili changamoto mbali mbali za kimaisha,kujenga umoja na kutengeneza fursa za kimaendeleo, kitaaluma na ikiwa ni pamoja na kusaidiana.
  
2.   DIRA
Kuona kwamba maslahi ya wanachama yanaboreshwa, kushirikiana na kuhakikisha shule inakua na ustawi mzuri kimazingira na kielimu.
  
3.   MIPAKA
  • Awe amesoma Arusha Sekii au aliwahi kusoma Arusha Sekii
  
4.   MASHARTI
  • Awe anatoa michango yake ( ada ya kujiunga na ada ya kila mwaka)
  • Awe anahudhuria vikao bila kukosa, na atakae kosa vikao vitatu mfululizo atakua amejitoa mwenyewe.
  • Mwanachama alifutiwa uanachama akitaka kujiunga tena itamlazimu kuandika barua na barua itajadiliwa na wanachama wote
  
5.   KUJIUNGA
  • Kila mwanachama atatakiwa kujaza form na kuleta picha moja (passport size)
  • Ada ya kujiunga ni – TZS 20,000 ( SHILINGI ELFU ISHIRINI TU)
  • Ada ya form ni – TZS 2,000 ( SHILINGI ELFU MBILI TU)
  • Ada ya mwaka ni – TZS 50,000 (SHILINGI ELFU HAMSINI TU)
     (fomu zote zitapatikana kwa katibu wa kila mkoa, fomu zitakazo kubalika ni zenye muhuri wa kikundi)
  
6.   MUDA WA VIONGOZI
  • Viongozi watakua madarakani kwa kipindi cha miaka miwili. Ili viongozi warudie uongozi watatakiwa kupumzika kwa kipindi cha miaka miwili.
  
7.   UCHAGUZI WA VIONGOZI
  • Viongozi wote watapendekezwa na wanachama na kupigiwa kura


  
8.   MAMBO YASIOKUBALIKA
  • Mambo yasiokubalika katika kikundi hiki ni kama ifuatavyo: siasa,Udini, Ukabila, Lugha chafu, Matusi na utani uliovuka mipaka.
  
9.   MAMBO YANAYOKUBALIKA
  • Kupashana habari katika jambo lolote nje ya mambo yalioelewa hayaruhusiwi.
  • Kusaidiana katika shida na raha



10.  MIKUTANO YA KIKUNDI
  • Mikutano ifanyike siku moja  na Kutakua na mikutano mara 6   (SITA) kwa kila mwaka ambayo itafanyika kila jumamosi ya mwisho wa mwezi kama itakavyotangazwa na katibu.
  
11.                    MIPANGO YA BAADAE
  • Kua na ofisi
  • Kuanzisha mradi wa kikundi/ SACCOS
  • Kujireka karibu na shule ili kupambana na changamoto zinazoikabili.



  
12.                    REPOTI YA KIKUNDI
  • Repoti ya mahesabu ya kikundi itatakiwa kutolewa mara tatu (3) kwa mwaka na kusomwa katika kikao mbele ya wanachama kutoka kwa mweka hazina

B:  UFUNGUZI WA ACCOUNT
  • Wanachama walijadiliana na kukubaliana kufungua account ya hundi katika Benki ya FBME,sababu ya kufingua account katika benki hiyo ni, hakuna ukiritimba na kuna uwezo wa kuona statement online.
  • Wanachama waliwachagua wawaweka sahihi katika akaunt hiyo kuwa ni:
    • Joshua – Mwenyekiti
    • Hellen Kasegenya – Mweka hazina
    • Julieth Kichao – Mwanachama

  • Ambapo katika utoaji wa fedha itahitajika sahihi ya wote watatu katika kila hundi.

C: SHEREHE KATIKA VIKUNDI
 kutakua na siku mbili kwa mwaka za kufanya sherehe kwa ajili ya kikundi cha  Wana Arusha Sekii, ambapo siku moja itakua rasmi kwaajili ya kumuenzi muasisi wa Arusha sekii ( ifanyike katika mwezi alioanzisha kikundi cha Arusha Sekii Kwenye Facebook). Kikundi kitakua na dhamana ya kugharamia safari yake( nauli, malazi na chakula)

wanachama wote watatakiwa kuchangia kiasi cha fedha zitakazo hitajika kwaajili ya kuadhimisha sherehe hizo.

D. SHEREHE YA KUFUNGA MWAKA ( GET TOGETHER PARTY)  NA UJIO WA MGENI

  • Wanachama waafikiana kuwe na sherehe kipindi mgeni wetu Aloyce Mbullu atakapo kuja mwezi wa November 2011.
  • Kila mwanachama atakae penda kuudhuria sherehe hizi atatakiwa kutoa mchango wa TZS 20,000/=
  • Muda wa kutoa fedha hizi ni kuanzia tarehe 1/10/2011 hadi 31/10/2011

E. NJIA YA KUWASILISHA ADA NA MICHANGO YOYOTE
  • Kupitia account ya kikundi
Kila mwanachama atakaeweka fedha zake benki anaombwa kuhakikisha ameandika jina lake kwenye risiti ya benki na kumuomba mhudumu wa benki aandike jina lake. Hii itaturahisishia kujua nani ametoa michango yake na nani bado. Pia risiti zote zitatakiwa kumfikia mweka hazina kwaajili ya kuhifadhi kumbukumbu.



  • M-PESA
Namba ya wakala – 40761 – EMA MROSSO JAZZ PROMOTION
 Kwa yeyote atakaetumia M-PESA tunaomba atumie simu yake ili tuweze kupata jina kamili ya mwanachama. Na kwa Yule atakaetumua simu ambayo sio yake tafadhali ujumbe mfupi kupitia namba 0754 004223

  • Kupeleka moja kwa moja kwa mweka hazina, KASEGENYA & COMPANY , Namba ya simu – 0754 288768
Au
Kupeleka Dukani kwa katibu, SINCA COURT HOTEL room no. 7. Namba ya simu- 0754 004223 ( hapa utamkuta dada anaitwa GABRIELA au EMMA utampatia jina lako na mwaka uliomaliza, hakikisha amekupatia risiti)


  • MAJUKUMU
  1. ADA YA MATANGAZO – DrJoseph R. Kingo
  2. RISITI/MHURI STATIONARY- Hellen kasegenya
  3. MAWASILIANO NA MAMA MLOWASA – Anna Denis
 

Kikao kilifungwa rasmi hadi jumamosi tarehe 29/10/2011 saa nane kamili – ARUSHA NIGHT PARK (MAKABURINI/REST IN PEACE)

Wednesday, September 28, 2011

TAARIFA YA KIKAO JIMBO LA DAR ES SALAAM 25/09/2011


MUHTASARI WA KIKAO CHA PILI CHA JUMUIYA YA ARUSHA SEKONDARI ( SEKII) JIMBO LA DAR ES SALAAM KILICHOFANYIKA MZALENDO PUB JUMAPILI YA TAREHE 25/ 9/ 2011.

                                                    MAHUDHURIO:

             JINA                                          MWAKA

  1. IRENE WALALA                                   1996
  2. SAID MUYA                                          1995
  3. SAMUEL MPONEZYA                         1996
  4. HASHIM ABDUL                                  1994
  5. LINNUS CHALAMILA                         1993
  6. PETER MGASSA                                   1994
  7. DAUDI MAVURA                                  1994
  8. BAKARI SEIF                                        1995
  9. JONAS JOSEPH                                    1996
  10. KISAKA MAVOA                                  1994
  11. BARIKI MWASAGA                              1993 (Form one)
  12. MARTIN MBOTO                                  1993
  13. TUMAINI LEONARD KIMATHI           1994
  14. JACOB LABAN SUMARY (KISALI)    1994
  15. ATUPELE MWAKALINGA                    1996

WALIOTOA UDHURU

  1. GRACE SHILIWA
  2. AMON ELISHA
  3. ABEL LASWAI
  4. ZUHERI ZAHORO

AGENDA 

  1. Kufungua Kikao,
  2. Uongozi,
  3. Katiba,
  4. Kuongeza nguvu ya jumuiya
  5. Mengineyo, na
  6. Kufunga Kikao.

KUFUNGUA KIKAO
Kikao kilifunguliwa na Mwenyekiti wa muda Bw Daudi Mavura kwa kuwakaribisha wajumbe katika kikao hiki na kuwaomba waweze kushiriki kikamilifu.  Baada ya kuwakaribisha wajumbe, Mwenyekiti aliruhusu agenda za kikao zitengenezwe, wajumbe kwa pamoja walikubaliana juu ya agenda za kikao husika.


UONGOZI
Wajumbe walipendekeza kuwa na viongozi wa mpito ambao watakuwa wanashirikiana moja kwa moja na viongozi walioko Arusha. Kwani wana jumuiya walioko Arusha na wa hapa Dar lengo letu ni moja, kuna umuhimu wa kuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na wenzetu walio nje ya Dar. Baada ya hoja za muda mrefu, wajumbe walikubaliana kuwa tuanze na Katiba ya Umoja huu na mengine yatafuata.

KATIBA
Ilipendekezwa kuwa jumuiya yetu iongozwe na Katiba.  Sifa, majukumu na jinsi ya kupata wanachama,viongozi, washauri, wakurugenzi n.k vyote vitakuwa ndani ya katiba. Katiba itakuwa ndiyo muongozo wa shughuli zote za jumuiya yetu. Tukifanikiwa kuwa na katiba nzuri, na tukiweza kuisajili BRELA na Wizara ya Mambo ya Ndani basi utakuwa ni mwanzo mzuri wa maendeleo ya jumuiya yetu. Makampuni mbalimbali ya ndani na nje ya nchi yanaweza kutusaidia endapo tutakuwa na jumuiya iliyosajiliwa kisheria. Ili kufanikisha upatikanaji wa Katiba, iliundwa timu ya watu watatu ambao ni kama ifuatavyo:-
                               i.           Jonas Joseph.                     
                               ii.           Hashim Abdul, na    
                               iii.            Atupele Mwakalinga.
Wanatakiwa waandae  rasimu ya kwanza (first draft) ya katiba yetu na kikao kijacho waje nayo. Ila waliambiwa ni vyema tarehe 15/ 10/2011 rasimu ya kwanza iwe tayari.

KUONGEZA NGUVU YA JUMUIYA
Baadhi ya wajumbe walikiambia kikao kuwa waliwahi kusikia kuwa kuna wenzetu wa Arusha Sekondari nao wana umoja wao hapa Dar. Hivyo ikapendekezwa kuwa ni bora tuwatafute na tuwashirikishe katika shughuli za Jumuiya yetu. Hivyo basi tuliwaomba Kaka Tumaini Kimathi na Peter Mgasa waweze kuwatafuta.

  MENGINEYO
i.  Ilielezwa kuwa kuna pengo (mahusiano yasiyo mazuri sana) kati ya waalimu wa O- level na A- level  hivyo basi kuna umuhimu wa  Jumuiya yetu kutoegemea upande wowote. Pia ilipendekezwa kuwa  kama kuna walimu ambao wanafundisha Sekii na ambao walisoma pale basi ni vyema tuwashirikishe nao wawe ni wanajumuiya.

  ii.  slogan ya jumuiya yetu iliundwa ambayo ni

Mmoja anaita………….Sekiii
Mnaitikia…………………Pamoja
Anaita tena……………..Pamoja
Mnajibu…………………..Tunaweza
Wote mnamalizia………ngaaa!!!!!! (nukta ya peter mgasa)
Hii inasaidia kuamsha waliolala, kuleta morali katika utendaji kazi.

 iii.   Kuna umuhimu wa sisi kujitangaza na kuwa picha katika jamii kwa kutenda mambo mema yenye manufaa kwa jamii yetu na hasa kwa jumuiya ya Sekii.

 iv.  Kuna umuhimu wa kuwa na mission nyingi zitakazotuunganisha pamoja na siyo kupiga rangi baadhi ya majengo tu .Suala la msingi ni kujua hitaji la Shule la msingi ni lipi na jinsi ya kulitatua. Mission zetu pia zilenge manufaa ya wanajumuiya, ni muhimu wigo kupanuliwa na  hata kuhusisha masuala ya kifamilia.

v.   Pia wajumbe walijulishwa kuwa Jumuiya yetu inakua na itaendelea kukua, hivyo ni bora kuwa na mipango bora ya baadae.

vi.  Baada ya kuwa na kikundi kilichosajiliwa, tuwaweza kuwasiliana na makampuni mbalimbali mfano voda, tigo, airtel nao itakuwa ni rahisi kutusaidia kama jumuiya.

vii. Umuhimu wa kuwa na official website na pia italetwa hapa jinsi ya kuiboresha na itakuwa na rangi za shule yetu na Ndugu Samwel Mponezya  ataishughulikia.   Wajumbe walikubaliana kuwa suala la website liwekwe pembeni mpaka jumuiya yetu itakapoimarika, kwa sasa tuendelee kutumia blog na facebook.

viii. Blog inaendelea kuwa chini ya Dr. Kingo mpaka hapo website itakapokuwa tayari. Kuna umuhimu wa kuwafungia watu wanaochafua hali ya hewa  katika facebook group yetu (wasiofuata misingi na kanuni za jumuiya yetu).

 ix. Mawasiliano yaboreshwe na siyo kupitia facebook tuu, tuweze kutuma na sms pia kwa kuwa bado walio facebook ni wachache kuliko wasio.

Aidha kikao kilipitia taarifa ya kikao cha pili cha Jimbo kuu la Arusha na kupendekeza kama ifuatavyo:mapendekezo yameandikwa kwa wino mzito(red) na italic

MADA;
1.Imeamuliwa kuwa kutakuwa na Ada ya uanachama(members fee) kwa kila mwanachama ambayo ni 20,000(elfu ishirini) pesa halali na taslimu za kitanzania, au kwa gharama hiyo hiyo kwa pesa za kigeni.Wajumbe wote waliohudhuria vikao viwili na walio toa udhuru  wanakua ni waanzilishi rasmi wa jumuiya ya Arusha Sekii na watakua wameingia moja kwa moja bila kutoa ada hiyo.Kikao kilipendekeza pia kuwa utaratibu huu utumike katika mikoa,majimbo ama  nchi wajumbe  wanapokutana kwa ajili ya shughuli za jumuiya.

Ada ya uanachama iwe ni jukumu la kila mwanachama yaani mwanzilishi na mgeni. Hii itasaidia kuongeza kipato kwa taasisi yetu, pia kuwa na responsiuwajibikaji wa kila mwanachama. Kila anayemaliza shule ( form four au form six) anaruhusiwa kuwa mwanachama, ila lazima ajisajili na kuweza kulipa ada.  



2.kutembelea uongozi wa shule ya Sekondari ya Arusha na kuweka wazi dhumuni letu ili jumuiya yetu iweze Kutambulika rasmi. Hii itatusaidia hata tutakapo kuwa tunahitaji kufanya michango(fund rising), na pia kama tutataka kushirikisha mashirika mengine ili kutoa michango yao, au tukiwa tuna misaada kutoka nje ili iwe rahisi kuingia nchini bila kulipiwa ushuru kwani taratibu zote zitafuatwa kwa urahisi na vifaa vya shule havitozwi ushuru.
- Pia kujadili na uongozi wa shule kuona nini wangependa jumuiya iwafanyie.


Jimbo la Dar es Salaam limeafiki pendekezo hilo.


3. Kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja baina ya wajumbe ili kufahamiana vizuri kwa karibu zaidi,pia kutakuwa na form ambazo kila mwanachama anaejiunga atatakiwa kukamilisha ili tuweze kupata na kutunza kumbu kumbu  zake zote. na rekodi hizo zitahifadhiwa na katibu.

Jimbo la Dar linaafiki mapendekezo haya, ila hizo fomu na masharti ya kuwa mwanachama yatakuwa ndani ya Katiba

4.Kumpokea mwanajumuiya wa jimbo la Marekani DC(Aloyce Mbullu susa) ambaye anategemewa kuwasili nchini mapema mwanzoni mwa mwezi wa kumi na moja mwaka huu.pia kuweka mikakati ya malengo ya haraka,muda mfupi na mrefu.


 Jimbo la Dar linaafiki mapendekezo hayo.

5. Faida kwa wanachama
- kufahamiana
-kusaidiana katika raha na matatizo
-kubadilishana mawazo
-kujenga umoja na udugu

 Faida zimekubaliwa na Jimbo la Dar es Salaam.



6. mahudhurio kwenye vikao
Mwanachama yeyote asiehudhuria vikao mara tatu bila kutoa udhuru atatakiwa kulipa tozo.

 Jimbo la Dar limeridhia

KUFUNGA KIKAO
Kikao kiliahirishwa na Mwenyekiti mpaka jumapili ya tarehe 6 Novemba, 2011 pale DDC Mlimani city na Bwana Kisali ataratibu.

Mwenyekiti                                               Katibu

………………….                                   ………………………
Daudi Mavura                                   Atupele Mwakalinga

Wednesday, September 21, 2011

WANAJUMUIYA WA KANDA ZA ARUSHA NA DAR ES SALAAM WAFANYA MIKUTANO.

Wanajumuiya wa kanda ya Arusha na wale wa kanda ya Dar es salaam wanatarajia kufanya mikutano katika kanda zao siku ya jumapili 25/09/2011.Mkutano wa Arusha utafanyikia kuanzia saa nane mchana katika hotel ya Olduvai Inn mjini Arusha wakati ule wa kanda ya Dar utafanyika kuanzia saa kumi jioni.mikutano hii ina lengo la kuboresha mikakati iliyofikiwa mwanzo ya kuona muungana katika jumuiya hii unakuwa na nguvu zaidi na pia kuweka muoanisho wa ajenda zilizojadiliwa katika vikao vilivyopita ili kutoa muda na kujadili mchakato wa kuunda katiba ya kudumu.Mkutano wa kanda ya Dar es salaam uliokuwa ufanyike siku moja kabla ya tarehe 25/09/2011 umeahirishwa kwa sababu zisizoweza kuzuilika na kupelekwa hadi tarehe hiyo.viongozi waandamizi wa kanda zote wamewataka wanajumuiya kuhudhuria vikao hivi bila kukosa ili kuweza kusonga mbele na ajenda zijazo.tunawatakia mikutano changanifu na pia kuwataka wana Arusha Sekii walioko katika nchi za marekani na ulaya kuiga mfano wa wahitimu wenzao kwa kuanza kujadiliana na kupeleka mapitio yao kwa ajili ya kurahisisha kutengenezwa kwa katiba yenye kuwanufaisha wana jumuiya wa kanda zote husika

Wednesday, September 14, 2011

WANAJUMUIYA WA KANDA YA ARUSHA WAFANYA UCHAGUZI







TAARIFA YA KIKAO CHA WAJUMBE WA JUMUIYA YA WAHITIMU WA SEKONDARI YA ARUSHA JIMBO LA ARUSHA 11/09/2011 OLDUVAI INN.


WALIOHUDHURIA


Gilda sangawe - 94
Hellen Kasegenya - 94
Emma Mrosso 95
Evelyne Amani -94
William joshua - 93
Wilfred Kadego - 2007
Bariki Mwasaga - 93
Anna Dennis Mushi - 94
Godwin sangawe -92
Amina rajabu - 97
Julieth kichau - 94
Neema Joshua[Ngerebe] - 94
Amani ngolugwa - 95


UDHURU

Alex Meng'olia 93.
Maymuna kirari.
Rechnald James.
Prisca shija.



AGENDA

Kuchagua viongozi

Viongozi walichaguliwa rasmi kama ifuatavyo kutokana na maamuzi ya kikao kilichopita.

MWENYEKITI; William Joshua
MWENYEKITI MSAIDIZI;Godwin Sangawe.

KATIBU; Emma Mrosso
 
KATIBU MSAIDIZI; Evelyne Amani

MWEKA HAZINA; Hellen Kasegenya
  
WARATIBU;

 Anna DeniS,
Amina Rajabu,
 Julius Makara.

MADA;

1.Imeamuliwa kuwa kutakuwa na Ada ya uanachama(members fee) kwa kila mwanachama ambayo ni 20,000(elfu ishirini) pesa halali na taslimu za kitanzania, au kwa gharama hiyo hiyo kwa pesa za kigeni.Wajumbe wote waliohudhuria vikao viwili na walio toa udhuru  wanakua ni waanzilishi rasmi wa jumuiya ya Arusha Sekii na watakua wameingia moja kwa moja bila kutoa ada hiyo. Na hii tunaomba na tunaomba utaratibu huu utumike katika mikoa ama  nchi wajumbe  wanapokutana kwaajili ya shughuli za jumuiya.

2.kutembelea uongozi wa shule ya Arusha Sekii na kuweka wazi dhumuni letu ili jumuiya yetu iweze Kutambulika rasmi. Hii itatusaidia hata tutakapo kuwa tunahitaji kufanya michango(fund rising), na pia kama tutataka kushirikisha mashirika mengine ili kutoa michango yao, au tukiwa tunamisaada kutoka nje itakua rahisi kuingia nchini bila kulipiwa ushuru kwani taratibu zote zitafuatwa kwa urahisi na vifaa vya shule havitozwi ushuru.
- Pia kujadili na uongozi wa shule kuona nini wangependa sisi tuwafanyie.

3. Kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja baina ya wajumbe ili kufahamiana kwa karibu zaidi,pia kutakuwa na form ambazo kila mwanachama anaejiunga atatakiwa kukamilisha ili tuweze kupata na kutunza kumbu kumbu  zake zote. na rekodi hizo zitahifadhiwa na katibu.

4.Kumpokea mwanajumuiya wa jimbo la Marekani(Aloyce Mbullu susa) ambaye anategemewa kutembelea nchini mapema mwezi wa kumi na moja mwaka huu.

5. Faida kwa wanachama
- kufahamiana
-kusaidiana katika raha na matatizo

6. mahudhurio kwenye vikao
Mwanachama yeyote asiehudhuria vikao mara tatu bila kutoa udhuru atatakiwa kulipa tozo.

7. mengineyo.
- hiki ni kikundi huru kisichohusiana na chama cha siasa chochote hapa nchini au nje ya nchi. kutakua hakuna siasa ya aina yeyote katika kikundi hiki.
- tunatakiwa kuwa na anwani maalum,website au blog na baadae ofisi kwa ajili ya jumuiya.
-Sherehe ndogo ifanyike na kikao kilipendekeza ifanyike kipindi mgeni wetu akiwa hapa.
- tuwe na program maalum kati ya wanachama wa Arusha sekii na Wanafunzi wa arusha seki.
-katiba- wanachama wote wapewe uhuru wa kujadili muongozo wetu tunaouhitaji. Na pia katiba yetu iwe inaweza kubadilika Ili kwenda na wakati.
- tuwe na ada ya kila mwaka kwa kila mwanachama. Hiki kiwe kiwango kidogo ambacho mwanachama yeyote ataweza kuchangia bila matatizo.
-matangazo ya biashara. kwa yeyote atakae taka kutangaza biashara yake atatakiwa kulipia Matangazo yake.

kutokana na muda kikao kilifungwa rasmi na Mwenyekiti Mh. William Joshua hadi tarehe 25/9/11 ambapo tutajadili kuhusu nidhamu,kuunda kamati ya nidhamu, na kupata viongozi watakao simamia kamati hiyp.Na pia tutajadiliana kuhusu mapokezi ya Ndugu Aloyce Mbullu.

Kwa niaba ya uongozi mzima wa jumuiya ninapenda kuwatakia wakati mwema na maandalizi mazuri ya kikao kinachokuja.Asanteni sana.

Miss Emma Mroso.
Katibu