KIKAO CHA PILI CHA ARUSHA SEKII ALUMNI (ASAA) KILICHOFANYIKA AICC CLUB TAREHE 28/01/2012
Kikao kilifunguliwa saa kumi na nusu jioni.
1. WALIOHUDHURIA
a. Evelyn Amani
b. Anna mushi
c. Hellen Kasegenya
d. Evans Shirima
e. Maria Mnzava
f. Gilda Sangawe
g. Veronica Joseph
h. Senorina John
i. Julius Makara
2. WALIOTOA TAARIFA
a. William Joshua
b. Godwin Sangawe
c. Oliva Kulwa
d. Dr. Joseph Kingo
3. KUSOMA MINUTES ZA KIKAO KILICHOPITA
3.1 Kamati zote zilizokuwa zimepewa kazi za kufanya zilitoa ripoti kama ifuatavyo:-
Kamati ya Sheria ilipewa kazi ya kukamilisha KATIBA.
3.1.1 Maria Mnzava aliripoti kuwa amejaribu sana kumtafuta Muheshimiwa Judith Lohay bila ya mafanikio. Aliomba watu wamsaidie kumtafuta akashauriwa ajaribu kumtafuta Joan amabaye ni dada yake Judith labda anaweza kutusaidia kumpata.
3.2 Kamati ya Uchumi na Mipango kuona Uongozi wa Shulekwa ajili ya kupaka rangi.
3.2.1 Waliohudhuria ni :-
Evelyn Amani
Anna Mushi
Julius Makara
Evans Shirima
Waliweza kumuona Mkuu wa Shule Msaidizi na kupewa maelekezo kuwa mambo yote ya shule kama hayapo chini ya bajeti ya Serikali hushughulikiwa na Bodi ya Shule, hivyo Kamati ilienda kumuona Mr. Shakir siku hiyo na kumueleza malengo ya wana jumuiya wa ASAA, nakutupokea kwa mikono miwili na kusema atashirikiana nasi. Alieleza baadhi ya matatizo yasiompendeza hapo shuleni ni kuahidiwa na Julius Makara kushirikiana nae kutatua matatizo hayo.
Mr. Shakir ni mjenzi na ana kampuni ya ujenzi hivyo imekuwa kazi rahisi kwetu maana anaenda mwenyewe kufanya survey ya majengo na kututumia quotation baada ya siku 2. Alisema atajaribu kutenganisha majengo katika Block 4 ilituweze kuangalia lipi tunaweza kuanza nalo.
3.3 Kamati ya Fedha, Kufungua akaunti ya wana ASAA.
3.3.1 Hawakuweza kwenda kufungua akaunti maana walikuwa wanasubiria barua kutoka Manispaa, Anna Mushi aliahidi kuishughulikia lakini alisema kuwa alishindwa kwasababu wahusika walipatwa na msiba hivyo wanaohusika na barua za aina hizo hawakuweza kupatikana.
Baada ya kujadili ikaonekana kuwa hatuhitaji barua tena hivyo akaunti itafunguliwa Joint Account Jumanne FBME Bank, watakaoenda ni Hellen Kasegenya, Evelyn Amani na Senorina John.
3.4 Kamati ya kufuatilia Form za kujiunga na kikundi
Wanaohusika ni Amani Golugwa na Anna Mushi, walituletea nakala ya Form iliokuwa tayari na tukaifanyia marekebisho kidogo, Evelyn Amani akaombwa akaifanyie kazi ya masahihisho hayo na kuiweka online kama inawezekana watu wakaiona moja kwa moja.
4. MASAHIHSHO YA MINUTES ZA KIKAO KILICHOPITA
4.1 Kipengele kinachosema Kamati zilizoundwa sehemu C. Kamati ya Fedha , kufungua akaunti, pesa iliyotolewa sh. 20,000/= ya kufungulia akaunti ilitolewa na Senorina John na sio Veronica Joshua kama ilivyoandikwa hapo mwanzo.
5. AGENDA MPYA
5.1 TUWE NA IDARA YA HABARI NA UENEZI
Hii itatusaidia kueneza Habari kuhusu jumuiya yetu na idara hii itakuwa inatupatia taarifa mbalimbali na hata kuupdate vitu vyote kwenye website yetu mpya.
5.2 WEBSITE
Tufanye juu chini website ianze kufanya kazi iliwakati tunaongea na watu iwe rahisi kwa kuingia na kuona kila kitu tulichokifanya na mpaka hapa tulipofikia. Waweze kuwa na mwamko wakujiunga na kuwa pamoja nasi.
5.3 FUNDRAISING/COCKTAIL PARTY
Wajumbe walikuwa na mawazo ya jinsi ya kupata pesa maana mambo ni mengi na hata tukishapata quotation inawezekana pesa zikahitajika nyingi na tukafikiria jinsi ya kupat a pesa itakuwa kwa njia ya kuandaa fund raising au cocktail party ya watu kuja na kushiriki nasi.
Jumamosi ya tarehe 4/02/2010 tutakutana saa tisa mchana AICC club kwa ajili ya kupanga jinsi ya kufany tuweze kupata fedha hizo za kukarabati shule.
Kikao kilifungwa saa kumi na moja na dakika hamsini na moja jioni.