Arusha Sekii Alumni
Kikao Cha Tarehe 26/01/2012
Kikao kilianza saa: 11:46 jioni
Walioudhuria:
1. William Joshua
2. Evans Shirima
3. Godwin Sangawe
4. Evelyn Amani
5. Gilda Sangawe
6. Anna Mushi
7. Senorina John
8. Hellen Kasegenya
9. Maguo Lusewa
10. Julius Makara
Waliochelewa:
1. Dr. Joseph Kingo a.k.a Nuhu Salehe
2. Emma Mroso
3. Amani Golugwa
4. Maria Mnzava
5. Daudi Mavura
6. Veronica Joseph
Waliomba Udhuru:
1. Ango Mwamafupa
2. Amina Rajabu
AGENDA:
1. Kujadili tathmini ya sherehe tuliyoifanya tarehe 21/01/2012.
2. Katiba
3. Mkakati wa mwaka huu wa 2012.
1. Tathmini ya Sherehe
- Bajeti ilikuwa nzuri sana lakini yenye mapungufu kidogo kutokana na matatizo yaliyojitokeza hapo katikati, hivyo wakati mwingine tujipange mapema na kwa mpangilio mzuri.
- Akaunti ya kikundi ifunguliwe mapema kuepuka maswala ya mtu kukaa na pesa mkononi.
- Taarifa kwa wana Sekii ifikishwe ipasavyo kwa muda, tuhakikishe tuna namba zote za wanachama na pia kama kuna jambo lolote wanachama wanapaswa kushiriki wataarifiwe wiki kabla na kukumbushwa siku moja kabla, hii itafanya watu wajipange vizuri hivyo maudhurio yatakuwa makubwa.
- Kazi ya pamoja ilikuwa nzuri sana maana tulikuwa tumepotezana kwa miaka mingi baada ya kumaliza shule lakini kazi iliyofanyika ikaonekana kama tuliokuwa pamoja siku zote. Mshikamano ulikuwepo.
- Wajumbe walizidi kusisitiza kuwa timu ilikuwa moja japo kulikuwa na vikwazo. Tuzidi kusonga mbele tusikwame. Pamoja tunaweza!
- Wajumbe walishauriwa kuheshimu muda, kwenye sherehe ilionekana wazi kuwa hatukwenda na muda vivyo hivyo hata kwenye vikao vyetu hatuzingatii muda. Hivyo basi kama tumeamua kubadilika basi tubadilike haswa kwenye swala hili la muda.
- Baadhi ya watu walitaka kudhibiti kikundi, ilishauriwa kuwa watu wakitoa maoni na kwa bahati mbaya ya kapingwa na wengi, itakuwa ni vyema wote tukubaliane nao. Tusianze kuleta mabishano na pia tukiamua kufanya kitu kizuri tuchangie tusivutane sana.
- Wajumbe walizidi kusisitiza kuwa tumeamua wote kwa pamoja tusonge mbele tusikate tama tutafika mahali tutasimama imara.
- Mwenyekiti alichangia kwa kusema kuwa japo na mapungufu yaliyokuwepo bado imeonekana tumejitahidi sana, uratibu ulikuwa sio mzuri ila shukrani ziende kwa watu wote walioamua kushikamana na kuwa na maamuzi ya pamoja. Pongezi nyingi zilienda kwa Hellen Kasegenya na Juliet Kichao kwa juhudi zao za hali na mali za kufanikisha sherehe hiyo. Kwa ujumla aliwapongeza wajumbe wote.
- Mweka Hazina alitusomea ripoti ya mapato na matumizi ya sherehe iliyopita akakabidhi nakala kwa Mwenyekiti na Katibu. Ripoti hiyo ilipitishwa na kupokelewa na wajumbe vizuri. Hatukuwa na deni lolote zaidi ya kukomboa picha. Tulipaswa kulipia sh.80,000/= fedha hizi zilichangwa na kukabidhiwa kwa mpiga picha na tukakabidhiwa Album na DVD kwa ajili ya ukumbusho.
Wafuatao walichanga pesa za kukomboa picha:-
I. William Joshua – 10,000/=
II. Juliana Makara – 10,000/=
III. Godwin Sangawe – 10,000/=
IV. Evans Shirima – 10,000/=
V. Senorina John – 5,000/=
VI. Hellen Kasegenya – 5,000/=
VII. Anna Mushi – 5,000/=
VIII. Gilda Sangawe – 5,000/=
IX. Daudi Mavura – 5,000/=
X. Maguo Lusewa – 5,000/=
XI. Emma Mroso – 5,000/=
XII. Dr. – 5,000/=
2. Katiba
- Baadhi ya wajumbe waliomba muda wa kujadili Katiba uongezwe ili watu wazidi kutoa maoni yao, lakini ilionekana kuwa tukiendelea kusubiri watu wajadili hatutakaa tuikamilishe mapema. Iliamuliwa kuwa Katiba ikabidhiwe kwa Muheshimiwa Judith Lohay atuunganishie zote mbili pamoja na kuileta kwetu ili tuipitie na kuchagua lugha ipi itumike.
3. Mkakati wa 2012 – Mwaka tunaupelekaje kwa ajili ya kutimiza malengo?
- Shule inaelekea kwenye miaka 50, tulikaa na kujadili tutaifanyia nini shule yetu. Kwanza tuliamua tusijichanganye na utaratibu wa shule sisi tuwe huru tujitegemee.
- mradi ulikwisha pangwa na wenzetu wa ughaibuni, moja ikiwa ni kupanga rangi shule na kuweka vio vipya pale ambapo tutakuta vilivyovunjika. Wenzetu wamejitoa kwa moyo na kuchanga kiasi cha karibu Euro 2000, hivyo nasi tuliombwa tujitoe kwa moyo tusiwaangushe wenzetu. Tuwaange mkono sana.
- Mwenyekiti alisema kuwa Mkuu wa Shule alikuwa na ombi lake la kujengewa ofisi lakini kutokana na kikundi chetu bado ni kichanga hatutaweza kufanya hivyo kwa sasa. Tunalikweka hili ombi lake kama malengo yetu ya muda mrefu.
- Mwakilishi wa Ughaibuni anaondoka tarehe 01/02/2012, hivyo tungependa aondoke na ripoti kamili ya kwenda kuwaeleza wenzetu walioko huko Ughaibuni mahali tulipofikia iliwasikate tama. Kwa kufanya hivy basi tuliunda kamati mbalimbali za kufuatilia mambo mbalimbali ili kufanikisha malengo yetu ya muda mfupi. Tuna muda kati ya sasa na mwezi wa sita.
- Kabla mjumbe ajaondoka nchini tumejipanga kufungua akaunti, tupake rangi shule na kurekebisha madirisha mabovu kwa kuweka mapya. Hapo hapo fomu nazo zitaandaliwa ataondoka nazo.
Kamati zilizoundwa:-
a.) Ya Kwanza ni KAMATI YA SHERIA ya kufuatilia KATIBA ikamilike nao ni:-
- Maria Mnzava (atatusaidia kupeleka kwa Muheshimiwa Judith Lohay)
- Judith Lohay
- Daudi Mavura (Atatusaidia kuipeleka kwa miradi Dar)
- William Joshua (Mwenyeliti)
b.) Ya Pili ni KAMATI YA UCHUMI NA MIPANGO, kuona Uongozi wa shule na kuomba muongozo ilituweze kupaka rangi shule na kutengeneza madirisha:-
- Evans Shirima
- Julius Makara
- Evelyn Amani
- Anna Mushi (ashughulikie pia barua ya kutoka Manispaa ili ituruhusu kufungua akaunti)
- Dr. Joseph Kingo
c.) Ya Tatu ni KAMATI YA FEDHA, kufungua akaunti FBME Bank:-
- Hellen Kasegenya
- Emma Mroso
- Juliet Kichao
Mpaka Jumatatu akaunti iwepo, wakati huo huo Mweka Hazina anaruhusiwa kupokea michango ya watu.
Veronica Joshua alitoa mchango wake sh.20,000/= wa kufungulia akaunti.
d.) Ya Nne ni KAMATI YA KUSHUGHULIKIA FOMU ZA KUJIUNGA:-
- Amani Golugwa
- Anna Mushi
Waratibu wote watashughulikia fomu hizi kwa pamoja. Bila kusahau nyuma ya fomu zinazoenda Ughaibuni zionyeshe Euro 20
Mwisho, mjumbe alitoa wazo kuwa Blog tuliyonayo sasa haina mvuto, sio rahisi pia kuitumia aliomba kama inawezekana ifanyiwe kazi iweze kuvutia na kuwa rahisi kuitumia. Evelyn Amani aliahidi kusajili domain ya kikundi na kutuma username na password kwa muhusika aweze kuweka mafile yetu hapo. Kama pia tungeweza kupata website designer ingekuwa vyema akatumia hiyo domain mpya.
www.arushasekii.or.tz itasajiliwa ijumaa 27/01/2012.
Kikao kilifungwa kwa kusisitiza kuwa tukikoseana tujifunze kusamhe na kusahau yaliyopita wote tuanze ukurasa mpya.
Kikao kingine kitakuwa Jumamosi tarehe 28/01/2012 saa tisa kamili mchana.
Kikao kilifungwa saa 2:25 usiku.