KIKAO CHA PILI CHA ARUSHA SEKII ALUMNI (ASAA) KILICHOFANYIKA AICC CLUB TAREHE 04/02/2012
Kikao kilifunguliwa saa 11:45 jioni.
1. WALIOHUDHURIA
a. Evelyn Amani
b. Anna Mushi
c. Hellen Kasegenya
d. Gilda Sangawe
e. Moses Adam
f. Julius Makara
g. Alex Kiondo
h. Ruben Samwel
2. WALIOTOA TAARIFA
a. Evans Shirima – Safarini Moshi
b. Senorina John – Msibani Usa river
c. Veronica Joseph - Safarini
d. Godwin Sangawe – Safarini Karatu lakini aliwahi kikao
e. Juliet Kichao – Anamuuguza baba yake mzazi
3. KUSOMA MINUTES ZA KIKAO KILICHOPITA
a. Katibu aliendesha kikao kwa niaba ya Mwenyekiti, tulipitia minutes za kikao kilicchopita na agenda mbili zikaongelewa
i) Ilikuwa taarifa ya kufungua akaunti naye Hellen akatupatia taarifa zifuatazo:-
- Watu wawili wanahitajika kufungua Joint akaunti
- Wanahitaji kuwa na Reference letter kila mmoja
- Kitambulisho cha Kazi /Kitambulisho cha mpiga kura / Passport
- Residential proof kila mmoja/ barua kutoka kwa Mtendaji
- Passport size pictures kila mmoja.
- Starting /Minimum balance ya akaunti ni Sh.300,000/=
- Kikundi kikishasajiliwa then tunaweza kuhamisha kwenda kwenye jina la kikundi.
- Waliochaguliwa kwenda kufungua hiyo Joint akaunti ni Hellen Kasegenya na Evelyn Amani.
- Hivyo watu wote walihimizwa waanze kulipia ada zao za registration tuweze kwenda kufungua hiyo akaunti wakati huo huo wanaoweza kukamilisha Annual fee zao wanaruhusiwa kufanya hivyo maana mwisho ni mwezi wa tisa 2012.
- Waliotoa pesa zao za registration ni:-
1.) Julius Makara – 20,000/=
2.) Godwin Sangawe – 20,000/=
3.) Alex Kiondo -30,000/= (20,000 ya Registration na 10,000/= anaanza kulipia Annual fee )
4.) Hellen Kasegenya – 20,000/=
5.) Evelyn Amani – 20,000/=
Hivyo jumla mpaka sasa tunayo sh. 130,000/= ukijumlisha na ile Senorina aliyotoa siku za nyuma.
Watu walisistizwa watoa pesa ya kujiunga wakati form zinaendelea kufanyiwa marekebisho. Wanaweza kutuma kwa Mpesa kwa namba ya Hellen Kasegenya ambayo ni 0754288768
ii) Agenda nyingine iliyoongelewa ni Quotation iliyotumwa na Mwenyekiti wa Shule Mr. Shakir ilionekana nipesa nyingi sana ambayo tulihitaji wana Sekii wawepo kwa wingi tuweze kulijadili kuwa tutafanya nini, lakini wakati huo huo Mwana Sekii Moses alikuja na jambo linguine jipya ambalo lilikuwa Ombi kutoka kwa Mkuu wa Shule. Anahitaji kama tunaweza tukarabati darasa moja ambalo litakuwa French Lab, wamepata msaada kutoka Ufaransa na tarehe 20/02/2012 watakuwa hapa kwa ajili ya ufumbuzi na wangependa wakute darasa ni zuri lenye vioo, liwelimepigwa rangi na kuwekwa Mlango mzuri unaofunga.
Quotation zilizoletwa kwa ajili ya ukarabati huo, jumla yake ilikuwa sh. 1,314,980/=
Quotation hizo zilijadiliwa na hatimaye moses aliombwa aka draft vizuri na alihojiwa usafiri hivyo akirudi tena usafiri inabidi bei ipungue haikuwa halali na pia mlango bei yake ilikuwa juu sana. Atakyefuatilia maswala ya mlango Jeshini ni Ruben.
Hivyo inabidi tukutane wote kwa pamoja tena na kuwaeleza wenzetu wote kuwa jambo hili linahiyajika haraka na uongozi wa shule kama hili linawezekana basi Mkuu wa Shule atashukuru sana kama tutalifanikisha jambo hili kabla ya tarehe 20/02/2012.
Kikao kijacho tutakutana AICC Club tarehe 11/02/2012 saa 10:00 jioni.
Kikao kilifungwa saa 1:20 jioni.