KIKAO(ASAA) 17/06/2012.


KIKAO CHA (SABA) CHA ARUSHA SEKII ALUMNI (ASAA) KILICHOFANYIKA (AICC CLUB) TAREHE 17-06-2012

1.               WALIOHUDHURIA
a.      Joshua William
b.      Evelyn Amani
c.      Anna Mushi
d.      Evans Shirima
e.      Juliet Kichao
f.       Julius Makala


2.               WASIOHUDHURIA NA KUTOA TAARIFA
a. Hellen Kasegenya
b. Amani Golugwa
c. Seno
d. Goddy
e. Ango
f. Gilda


3.0         KUFUNGUA KIKAO

               Kikao kilifunguliwa na Mwenyekiti, na kutupatia agenda zifuatazo:-


3.1   Swala la kuhusu Mweka Hazina
-        Mwenyekiti alitupatia taarifa kuwa Mweka Hazina wetu (Hellen Kasegenya) amepata uhamisho anahamia Dar-es-salaam hivyo hatunabudi kumchagua Mweka Hazina mpya. Mapendekezo yalipitishwa kuwa Mweka Hazina wetu mpya atakuwa Juliet Kichao.
-        Mweka Hazina mpya aliombwa awasiliane na Hellen Kasegenya aweze kukabidhiwa michango ya wana Arusha Sekii waliokwisha kuchangia kwa ajili ya kufungua akaunti.
-        Wakati huo huo Evans Shirima aliombwa atusaidie kufuatilia masharti ya kufungua akaunti TWIGA BANCORP ilituweze kufungua akaunti hiyo haraka iwezekanavyo.
-        Tuliweza pia kumchagua Katibu msaidizi ambaye ni Amani Golugwa.
Hivyo viongozi ni kama wafuatavyo:-
a.      Joshua William – Mwenyekiti
b.      Evelyn Amani – Katibu
c.      Amani Golugwa – Katibu Msaidizi
d.      Juliet Kichao – Mweka Hazina
e.      Anna Mushi – Mratibu
f.       Julius Makala – Mratibu Msaidizi

3.2   Katiba – Tulitaka kujua watu wa Dar wamefikia wapi na kuregister chama chetu, Anna Mushi ataenda Dar wiki hii hivyo aliombwa kufuatilia jambo hili na ajitahidi tuweze kufanikisha jambo hili.

3.3   Muelekeo wa Kikundi – Mwenyekiti aliongelea juu ua ku plan juu ya kikundi chetu. Tuhakikishe tuna short and long term goals ilituweze kufanikiwa. Tulikuwa na malengo mengi lakini hata moja hatujakamilisha. Tulitakiwa wana Arusha Sekii wote tuwe tumeshatoa sh. 20,000/=kila mmoja wetu ilituweze kufungua akaunti na tulisema hivyo ndivyo viingilio lakini hadi wa leo ni wachache sana waliokwisha fanya hivyo. Tunahitajika pia ifikapo mwezi wa tisa mwaka huu 2012 tuwe tumekamilisha ada ya mwaka sh. 50,000/= lakini bado hatujafanya hivyo. Tunahitaji kusimama imara na kuhamasisha watu watoe michango yao tuweze kusonga mbele.




4.0         MENGINEYO

a.      Ilishauriwa kuwa pesa tunazokusanya zisikae mikononi kwa mtu, pesa yote ipelekwe bank                       
kwenye akaunti ya wana Sekii. Wenzetu walioko Dar wangependa kujua tumefikia wapi na kufungua akaunti, tujitahidi tuifungua haraka iwezekanavyo.

b.      Uhamasishaji wa wana ASAA wa kuja kwenye vikao. Tumeonelea tusiwe kila siku ni kutoa mawazo ya vitu vya kufanya inabidi pia tuwe tunakaribisha watu kwenye burudani mbalimbali ili tuweze kufahamiana zaidi. Tuongeze Entertainments za kutosha ili tusichoke vikao, na pia tuwetunabadilisha sehemu mbalimbali pakukutania.  Ikapitishwa kuwa next meeting place itakuwa TEMBO Club – KISONGO. Na hii itakuwa the coming Saturday tarehe 23/06/2012.

c.      Kuzindua Mfuko wa jamii, tumeonelea ni jambo la busara, tunasaidiana katika shida pia tungependa tuwe na mfuko wa kusaidiana, tukiwa tunakutana hata ukija na kiasi cha sh. 1000/= kwa ajili ya mfuko wa jamii wa kusaidiana haitakuwa vibaya. Tutaliongelea vizuri jambo hili tukiwa TEMBO CLUB.

d.      Matangazo kwenye Radio na gazeti la Arushatimes, tumeonelea haitakuwa jambo baya vikao vijavyo tuingie gharama ya kutangaza kwenye radio mbalimbali na gazeti la Arushatimes ilituweze kupata maudhurio mazuri kwenye vikao. Ujumbe wa sms tunaona haufikii watu wengi lakini ukitangaza kwenye radio zinazosikilizwa sana mjini Arusha watu wanaweza kupata taarifa.

e.      Social day, Tuliamua kuwa in September 2012 lazima tufanye Sekii Gathering, mahali na muda tutawatangazia baadaye.

f.       Ugonjwa, tunamwana Sekii mwenzetu aliugua ghafla na kwa taarifa tulizonazo anaendelea vizuri huyu ni Hashim Abdul alioko Dar-es-salaam. Mwenye chochote akiwakilishe kwa Anna Mushi akiwa Dar anaweza kumtafuta na kumpatie pole zetu. Pia tuna mwenzetu mwingine anayeuguliwa na Mzazi wake (Baba) hapa Arusha naye ni Irene Walala pia ukipata muda unaweza kwenda kumpatia pole pale Selian (ALMC) Hospital.

5.0         KUFUNGA KIKAO

Tulifunga kikao kwa kuombeana mema na kukumbushana tujitahidi tufungue akaunti na pia kuhamasisha watu waje kwenye vikao.

Kikao kilifungwa saa kumi na mbili na nusu jioni.

2 comments:

Anonymous said...

That's very good, katibu, kazi inaonekana na inasomeka, sasa ni rahisi kufanya hata follow ups.
William

ARUSHA SEKII ALUMNI said...

safi sana na hongereni sana kwa mawazo na michango mizuri.mimi binafsi ninasisitiza sana swala la katiba kwa sababu sasa imekuwa ni muda mrefu sana swala hili bado hatujalimaliza,wito kwa mwenyekiti wa jimb la Dar kuhakikisha katiba inakamilika mampema ili tuweze kutafuta wafadhili.
Dr J Kingo