MUHTASARI WA KIKAO CHA PILI CHA JUMUIYA YA ARUSHA SEKONDARI ( SEKII) JIMBO LA DAR ES SALAAM KILICHOFANYIKA MZALENDO PUB JUMAPILI YA TAREHE 25/ 9/ 2011.
MAHUDHURIO:
JINA MWAKA
- IRENE WALALA 1996
- SAID MUYA 1995
- SAMUEL MPONEZYA 1996
- HASHIM ABDUL 1994
- LINNUS CHALAMILA 1993
- PETER MGASSA 1994
- DAUDI MAVURA 1994
- BAKARI SEIF 1995
- JONAS JOSEPH 1996
- KISAKA MAVOA 1994
- BARIKI MWASAGA 1993 (Form one)
- MARTIN MBOTO 1993
- TUMAINI LEONARD KIMATHI 1994
- JACOB LABAN SUMARY (KISALI) 1994
- ATUPELE MWAKALINGA 1996
WALIOTOA UDHURU
- GRACE SHILIWA
- AMON ELISHA
- ABEL LASWAI
- ZUHERI ZAHORO
AGENDA
- Kufungua Kikao,
- Uongozi,
- Katiba,
- Kuongeza nguvu ya jumuiya
- Mengineyo, na
- Kufunga Kikao.
KUFUNGUA KIKAO
Kikao kilifunguliwa na Mwenyekiti wa muda Bw Daudi Mavura kwa kuwakaribisha wajumbe katika kikao hiki na kuwaomba waweze kushiriki kikamilifu. Baada ya kuwakaribisha wajumbe, Mwenyekiti aliruhusu agenda za kikao zitengenezwe, wajumbe kwa pamoja walikubaliana juu ya agenda za kikao husika.
UONGOZI
Wajumbe walipendekeza kuwa na viongozi wa mpito ambao watakuwa wanashirikiana moja kwa moja na viongozi walioko Arusha. Kwani wana jumuiya walioko Arusha na wa hapa Dar lengo letu ni moja, kuna umuhimu wa kuwa na mawasiliano ya mara kwa mara
na wenzetu walio nje ya Dar. Baada ya hoja za muda mrefu, wajumbe walikubaliana kuwa tuanze na Katiba ya Umoja huu na mengine yatafuata.
KATIBA
Ilipendekezwa kuwa jumuiya yetu iongozwe na Katiba. Sifa, majukumu na jinsi ya kupata wanachama,viongozi, washauri, wakurugenzi n.k vyote vitakuwa ndani ya katiba. Katiba itakuwa ndiyo muongozo wa shughuli zote za jumuiya yetu. Tukifanikiwa kuwa na katiba nzuri, na tukiweza
kuisajili BRELA na Wizara ya Mambo ya Ndani basi utakuwa ni mwanzo mzuri wa maendeleo ya jumuiya yetu. Makampuni mbalimbali ya ndani na nje ya nchi yanaweza kutusaidia endapo tutakuwa na jumuiya
iliyosajiliwa kisheria. Ili kufanikisha upatikanaji wa Katiba, iliundwa timu ya watu watatu ambao ni kama ifuatavyo:-
i. Jonas Joseph.
ii. Hashim Abdul, na
iii. Atupele Mwakalinga.
Wanatakiwa waandae rasimu ya kwanza (first draft) ya katiba yetu na kikao kijacho waje nayo. Ila waliambiwa ni vyema tarehe
15/ 10/2011 rasimu ya kwanza iwe tayari.
KUONGEZA NGUVU YA JUMUIYA
Baadhi ya wajumbe walikiambia kikao kuwa waliwahi kusikia kuwa kuna wenzetu wa Arusha Sekondari nao wana umoja wao hapa Dar. Hivyo ikapendekezwa kuwa ni bora tuwatafute na tuwashirikishe katika shughuli za Jumuiya yetu. Hivyo basi tuliwaomba Kaka
Tumaini Kimathi na Peter Mgasa waweze kuwatafuta.
MENGINEYO
i. Ilielezwa kuwa kuna
pengo (mahusiano yasiyo mazuri sana) kati ya waalimu wa O- level na A- level hivyo basi kuna umuhimu wa Jumuiya yetu kutoegemea upande wowote. Pia ilipendekezwa kuwa kama kuna walimu ambao wanafundisha Sekii na ambao walisoma pale basi ni vyema tuwashirikishe nao wawe ni wanajumuiya.
ii. slogan ya jumuiya yetu iliundwa ambayo ni
Mmoja anaita………….Sekiii
Mnaitikia…………………Pamoja
Anaita tena……………..Pamoja
Mnajibu…………………..Tunaweza
Wote mnamalizia………ngaaa!!!!!! (nukta ya peter mgasa)
Hii inasaidia kuamsha waliolala, kuleta morali katika utendaji kazi.
iii. Kuna umuhimu wa sisi kujitangaza na kuwa picha katika jamii kwa kutenda mambo mema yenye manufaa kwa jamii yetu na hasa kwa jumuiya ya Sekii.
iv. Kuna umuhimu wa kuwa na mission nyingi zitakazotuunganisha pamoja na siyo kupiga rangi baadhi ya majengo tu .Suala la msingi ni kujua hitaji la Shule la msingi ni lipi na jinsi ya kulitatua. Mission zetu pia zilenge manufaa ya wanajumuiya, ni muhimu wigo kupanuliwa na hata kuhusisha masuala ya kifamilia.
v. Pia wajumbe walijulishwa kuwa Jumuiya yetu inakua na itaendelea kukua, hivyo ni bora kuwa na mipango bora ya baadae.
vi. Baada ya kuwa na kikundi kilichosajiliwa, tuwaweza kuwasiliana na makampuni mbalimbali mfano voda, tigo, airtel nao itakuwa ni rahisi kutusaidia kama jumuiya.
vii. Umuhimu wa kuwa na official website na pia italetwa hapa jinsi ya kuiboresha na itakuwa na rangi za shule yetu na Ndugu Samwel Mponezya ataishughulikia. Wajumbe walikubaliana kuwa suala la website liwekwe pembeni mpaka jumuiya yetu itakapoimarika, kwa sasa tuendelee kutumia blog na facebook.
viii. Blog inaendelea kuwa chini ya Dr.
Kingo mpaka hapo website itakapokuwa tayari. Kuna umuhimu wa kuwafungia watu wanaochafua hali ya hewa katika facebook group yetu (wasiofuata misingi na kanuni
za jumuiya yetu).
ix. Mawasiliano yaboreshwe na siyo kupitia facebook tuu, tuweze kutuma na sms pia
kwa kuwa bado walio facebook ni wachache kuliko wasio.
Aidha kikao kilipitia taarifa ya kikao cha pili cha Jimbo kuu la Arusha na kupendekeza kama ifuatavyo:mapendekezo yameandikwa kwa wino
mzito(red) na italic
MADA;
1.Imeamuliwa kuwa kutakuwa na Ada ya uanachama(members fee) kwa kila mwanachama ambayo ni 20,000(elfu ishirini) pesa halali na taslimu za kitanzania, au kwa gharama hiyo hiyo kwa pesa za kigeni.Wajumbe wote waliohudhuria vikao viwili na walio toa udhuru wanakua ni waanzilishi rasmi wa jumuiya ya Arusha Sekii na watakua wameingia moja kwa moja bila kutoa ada hiyo.Kikao kilipendekeza pia kuwa utaratibu huu utumike katika mikoa,majimbo ama nchi wajumbe wanapokutana kwa ajili ya shughuli za jumuiya.
Ada ya uanachama iwe ni jukumu la kila mwanachama yaani mwanzilishi na mgeni. Hii itasaidia kuongeza kipato kwa taasisi yetu, pia kuwa na responsiuwajibikaji wa kila mwanachama. Kila anayemaliza shule ( form four au form six) anaruhusiwa kuwa mwanachama, ila lazima ajisajili na kuweza kulipa ada.
2.kutembelea uongozi wa shule ya Sekondari ya Arusha na kuweka wazi dhumuni letu ili jumuiya yetu iweze Kutambulika rasmi. Hii itatusaidia hata tutakapo kuwa tunahitaji kufanya michango(fund rising), na pia kama tutataka kushirikisha mashirika mengine ili kutoa michango yao, au tukiwa tuna misaada kutoka nje ili iwe rahisi kuingia nchini bila kulipiwa ushuru kwani taratibu zote zitafuatwa kwa urahisi na vifaa vya shule havitozwi ushuru.
- Pia kujadili na uongozi wa shule kuona nini wangependa jumuiya iwafanyie.
Jimbo la Dar es Salaam limeafiki pendekezo hilo.
3. Kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja baina ya wajumbe ili kufahamiana vizuri kwa karibu zaidi,pia kutakuwa na form ambazo kila mwanachama anaejiunga atatakiwa kukamilisha ili tuweze kupata na kutunza kumbu kumbu zake zote. na rekodi hizo zitahifadhiwa na katibu.
Jimbo la Dar linaafiki mapendekezo haya, ila hizo fomu na masharti ya kuwa mwanachama yatakuwa ndani ya Katiba
4.Kumpokea mwanajumuiya wa jimbo la Marekani DC(Aloyce Mbullu susa) ambaye anategemewa kuwasili nchini mapema mwanzoni mwa mwezi wa kumi na moja mwaka huu.pia kuweka mikakati ya malengo ya haraka,muda mfupi na mrefu.
Jimbo la Dar linaafiki mapendekezo hayo.
5. Faida kwa wanachama
- kufahamiana
-kusaidiana katika raha na matatizo
-kubadilishana mawazo
-kujenga umoja na udugu
Faida zimekubaliwa na Jimbo la Dar es Salaam.
6. mahudhurio kwenye vikao
Mwanachama yeyote asiehudhuria vikao mara tatu bila kutoa udhuru atatakiwa kulipa tozo.
Jimbo la Dar limeridhia
KUFUNGA KIKAO
Kikao kiliahirishwa na Mwenyekiti mpaka jumapili ya tarehe 6 Novemba, 2011 pale DDC Mlimani city na Bwana Kisali ataratibu.
Mwenyekiti Katibu
…………………. ………………………
Daudi Mavura Atupele Mwakalinga