TAARIFA YA KIKAO CHA WANAJUMUIYA WA ARUSHA SEKII JIMBO KUU LA ARUSHA 25/09/2011 OLDUVAI INN ARUSHA
MAHUDHURIO
William Joshua
Hellen Kasegenya
Emma Mrosso
Evelyne Amani
Julieth Kichao
Anna Denis
Mariam Mgonja
Senorina John
Kazeni Amini
UDHURU
Godwin Sangawe – Mwenyekiti Msaidizi
Wilfred Kadege
Shufaa Kaduni
Evans Shirima
Nazira Kassou
Gilda Sangawe
Jackline Masao
Amina Rajabu
AGENDA
A. KATIBA
Arusha sekii ni muungano wa hiari wa
1. LENGO
Kuwaunganisha kwa pamoja watu wote waliosoma Arusha Sekii na kujadili changamoto mbali mbali za kimaisha,kujenga umoja na kutengeneza fursa za kimaendeleo, kitaaluma na ikiwa ni pamoja na kusaidiana.
2. DIRA
Kuona kwamba maslahi ya wanachama yanaboreshwa, kushirikiana na kuhakikisha shule inakua na ustawi mzuri kimazingira na kielimu.
3. MIPAKA
- Awe amesoma Arusha Sekii au aliwahi kusoma Arusha Sekii
4. MASHARTI
- Awe anatoa michango yake ( ada ya kujiunga na ada ya kila mwaka)
- Awe anahudhuria vikao bila kukosa, na atakae kosa vikao vitatu mfululizo atakua amejitoa mwenyewe.
- Mwanachama alifutiwa uanachama akitaka kujiunga tena itamlazimu kuandika barua na barua itajadiliwa na wanachama wote
5. KUJIUNGA
- Kila mwanachama atatakiwa kujaza form na kuleta picha moja (passport size)
- Ada ya kujiunga ni – TZS 20,000 ( SHILINGI ELFU ISHIRINI TU)
- Ada ya form ni – TZS 2,000 ( SHILINGI ELFU MBILI TU)
- Ada ya mwaka ni – TZS 50,000 (SHILINGI ELFU HAMSINI TU)
6. MUDA WA VIONGOZI
- Viongozi watakua madarakani kwa kipindi cha miaka miwili. Ili viongozi warudie uongozi watatakiwa kupumzika kwa kipindi cha miaka miwili.
7. UCHAGUZI WA VIONGOZI
- Viongozi wote watapendekezwa na wanachama na kupigiwa kura
8. MAMBO YASIOKUBALIKA
- Mambo yasiokubalika katika kikundi hiki ni kama ifuatavyo: siasa,Udini, Ukabila, Lugha chafu, Matusi na utani uliovuka mipaka.
9. MAMBO YANAYOKUBALIKA
- Kupashana habari katika jambo lolote nje ya mambo yalioelewa hayaruhusiwi.
- Kusaidiana katika shida na raha
10. MIKUTANO YA KIKUNDI
- Mikutano ifanyike siku moja na Kutakua na mikutano mara 6 (SITA) kwa kila mwaka ambayo itafanyika kila jumamosi ya mwisho wa mwezi kama itakavyotangazwa na katibu.
11. MIPANGO YA BAADAE
- Kua na ofisi
- Kuanzisha mradi wa kikundi/ SACCOS
- Kujireka karibu na shule ili kupambana na changamoto zinazoikabili.
12. REPOTI YA KIKUNDI
- Repoti ya mahesabu ya kikundi itatakiwa kutolewa mara tatu (3) kwa mwaka na kusomwa katika kikao mbele ya wanachama kutoka kwa mweka hazina
B: UFUNGUZI WA ACCOUNT
- Wanachama walijadiliana na kukubaliana kufungua account ya hundi katika Benki ya FBME,sababu ya kufingua account katika benki hiyo ni, hakuna ukiritimba na kuna uwezo wa kuona statement online.
- Wanachama waliwachagua wawaweka sahihi katika akaunt hiyo kuwa ni:
- Joshua – Mwenyekiti
- Hellen Kasegenya – Mweka hazina
- Julieth Kichao – Mwanachama
- Ambapo katika utoaji wa fedha itahitajika sahihi ya wote watatu katika kila hundi.
C: SHEREHE KATIKA VIKUNDI
kutakua na siku mbili kwa mwaka za kufanya sherehe kwa ajili ya kikundi cha Wana Arusha Sekii, ambapo siku moja itakua rasmi kwaajili ya kumuenzi muasisi wa Arusha sekii ( ifanyike katika mwezi alioanzisha kikundi cha Arusha Sekii Kwenye Facebook). Kikundi kitakua na dhamana ya kugharamia safari yake( nauli, malazi na chakula)
wanachama wote watatakiwa kuchangia kiasi cha fedha zitakazo hitajika kwaajili ya kuadhimisha sherehe hizo.
D. SHEREHE YA KUFUNGA MWAKA ( GET TOGETHER PARTY) NA UJIO WA MGENI
- Wanachama waafikiana kuwe na sherehe kipindi mgeni wetu Aloyce Mbullu atakapo kuja mwezi wa November 2011.
- Kila mwanachama atakae penda kuudhuria sherehe hizi atatakiwa kutoa mchango wa TZS 20,000/=
- Muda wa kutoa fedha hizi ni kuanzia tarehe 1/10/2011 hadi 31/10/2011
E. NJIA YA KUWASILISHA ADA NA MICHANGO YOYOTE
- Kupitia account ya kikundi
- M-PESA
Kwa yeyote atakaetumia M-PESA tunaomba atumie simu yake ili tuweze kupata jina kamili ya mwanachama. Na kwa Yule atakaetumua simu ambayo sio yake tafadhali ujumbe mfupi kupitia namba 0754 004223
- Kupeleka moja kwa moja kwa mweka hazina, KASEGENYA & COMPANY , Namba ya simu – 0754 288768
Kupeleka Dukani kwa katibu, SINCA COURT HOTEL room no. 7. Namba ya simu- 0754 004223 ( hapa utamkuta dada anaitwa GABRIELA au EMMA utampatia jina lako na mwaka uliomaliza, hakikisha amekupatia risiti)
- MAJUKUMU
- ADA YA MATANGAZO – DrJoseph R. Kingo
- RISITI/MHURI STATIONARY- Hellen kasegenya
- MAWASILIANO NA MAMA MLOWASA – Anna Denis
Kikao kilifungwa rasmi hadi jumamosi tarehe 29/10/2011 saa nane kamili – ARUSHA NIGHT PARK (MAKABURINI/REST IN PEACE)

1 comment:
hongereni sana wajumbe kwa kazi nzuri tunaomba wajumbe wa majimbo mengine kutoa michango na maoni ya taarifa hii ili tuzidi kusonga mbele
DR J.Kingo
Post a Comment