Natumai wajumbe wezangu tuko salama,kabisa na pilika zetu za maisha ya kila siku,nimeweka kivuli cha katiba iliyoandaliwa na tume iliyoteuliwa kutoka Jimbo la Dar.unaweza kuipitia ukifuata ukurasa(page)ambayo inaonekana upande wa kulia kwako inayosomeka kama ifuatavyo.KATIBA YETU TOA MAONI.
naomba tutoe maoni ili kuboresha katiba hii na michango ya kukubaliana au kutofautiana nayo ili tuweze kufanya marekebisho na hatimaye tuwe na katiba rasmi.HII NI COPY TU YA KATIBA NA WALA SI KATIBA RASMI.ninawatakia tena wakati mwema na maandalizi mazuri ya siku kuu za Noel na Mwaka mpya.
Dr Joseph.Kingo
6 comments:
well katiba imejitosheleza kwenye sector zote hii ni kazi nzuri Dr.Kingo,nashukuru sana
1. hii katiba mbona iko km copy paste fulani. kwanini isiandikwe katiba ambayo itaendana na hali halisi ya jumuiya.
2. shule iko arusha, ofisi kuu iko Dar es salaam.kwanini ofisi kuu isiwe arusha , ambapo hata jumuiya ingeweza kuongea na uongozi wa shule kuomba ofisi hapo shuleni.
3.kwaujumla tu ningependekeza katiba hii iandikwe kwa njia ambayo itakua rahisi kueleweka kwa wanajumuia na pia bila kusahaulika kwa lengo na dira(mission and vision) ya jumuiya.
katiba iwe ya kiswahili wote tuelewe.
Nadhani tunahitaji kuwa na katiba inaand not copyyoenana na jumuiya yetu and paste of another org. na kutokana na shule kuwepo Arusha tulikubaliana tangu awali kwamba ofisi za jumuiya zitakuwa Arusha. Sijaelewa kama kuna kikao kingine kilikaa na kutengua maamuzi hayo, naomba nisaidiwe.
William Joshua
Mwenyekiti.
1.umeona eeeh mwk. hiki kizungu ni kingi na hakifai kitu kinachoanzishwa km hiki, hakifai kitu kinachohitaji watu kujiunga kwa hiari zao na hakinamahali kitakacho mhamasisha mtu kujiunga. nimuhimu kuzingatia mambo haya ili kupunguza nguvu za kuhamasisha watu. na pia itumike lugha inayoeleweka kwa wote kwani ninauhakika sio wote watakuwa na uwezo wa kuelewa kwa vizuri kunachoendelea.
2.Nadhani wengi wameelewa hili bomu sio lizuri ndio maana baada ya kulirusha watu wamekaa mbali kusikiliza mlipuko utakuwaje.
3. pia watu inaelekea wanajichanganya vibaya kwani utakuta watu waliyo udhuria vikao wakitoka huko wao ndio wako mstari wa mbele kupinga yale yaliozungumziwa pale huko kwenye hivyo vikao. je nikwamba watu hawapewi muda wa kutafakari au ni kwamba watu hawajachambui hoja kwa kina kabla ya kupitishwa.mfano mzuri utaona hata katiba inasema headoffice zake ziko dar hii ni kopy paste au ni mabadiliko kwa yale yote yaliokua yamezungumziwa. asanteni
Ofisi tulisema ziwe Arusha. Mwenyekiti William ndivyo tulivyokubaliana.
Amani Golugwa.
Post a Comment