Thursday, November 24, 2011

KATIBA

Ninapenda kuwakumbusha wajumbe wenzangu kuwa chanzo cha kupooza kwa hari iliyokuwapo mwanzo kuhusiana na jumuiya yetu unatokana(kwa maoni yangu) na kucheleweshwa pasipo sababu za msingi na mchakato wa katiba ambayo ndiyo mwongozo mama wa shughuli zetu,hivyo wanajumuiya wanachoka kusikiliza na kusoma mambo yasiyo ya msingi na  yanayopoteza muda mwingi sana na kutia maudhi,na badala yake kuhamia kwenye mambo mengine ambayo yanaonekana ni ya maana zaidi kwa maisha kuliko malumbano.Nina imani kabisa kama tutaanza upya kushughulikia katiba basi tutakuwa na mwamko na Ari ya kuchangia au hata kutokea kwenye vikao vyetu kama ilivyokuwa awali.basi ninatoa changamoto kwa majimbo mufti yanayoshughulikia swala la katiba kutupa mwanga wa wapi tumefikia na ni nini tunatakiwa kufanya ili tuwe na kitu cha kujadili kwa sababu bila ya kufanya hivyo tutabaki kuongea ni nani alimaliza mwaka gani na ni nani alipata alama gani kisha tutavuna kuchukiana na kubebeshana lawama pasipo kufahamu.Ninawatakia wakati mwema na shughuli njema hasa kwa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.
Dr J Kingo
mwenyekiti jimbo la ughaibuni

2 comments:

Sam said...

Umesomeka Dr, ngoja tubanane na katibu wetu hapa Dar (Atupele) na Jonas Tillya ambao ndio walipewa kazi ya kuratibu katiba ili kujua tulipofikia.

ARUSHA SEKII ALUMNI said...

nimefurahi kwa hilo mwana wa mponezya.nitanukuu makubaliano yetu ya kikao kama ifuatavyo

UONGOZI
Wajumbe walipendekeza kuwa na viongozi wa mpito ambao watakuwa wanashirikiana moja kwa moja na viongozi walioko Arusha. Kwani wana jumuiya walioko Arusha na wa hapa Dar lengo letu ni moja, kuna umuhimu wa kuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na wenzetu walio nje ya Dar. Baada ya hoja za muda mrefu, wajumbe walikubaliana kuwa tuanze na Katiba ya Umoja huu na mengine yatafuata.

KATIBA
Ilipendekezwa kuwa jumuiya yetu iongozwe na Katiba. Sifa, majukumu na jinsi ya kupata wanachama,viongozi, washauri, wakurugenzi n.k vyote vitakuwa ndani ya katiba. Katiba itakuwa ndiyo muongozo wa shughuli zote za jumuiya yetu. Tukifanikiwa kuwa na katiba nzuri, na tukiweza kuisajili BRELA na Wizara ya Mambo ya Ndani basi utakuwa ni mwanzo mzuri wa maendeleo ya jumuiya yetu. Makampuni mbalimbali ya ndani na nje ya nchi yanaweza kutusaidia endapo tutakuwa na jumuiya iliyosajiliwa kisheria. Ili kufanikisha upatikanaji wa Katiba, iliundwa timu ya watu watatu ambao ni kama ifuatavyo:-
i. Jonas Joseph.
ii. Hashim Abdul, na
iii. Atupele Mwakalinga.
Wanatakiwa waandae rasimu ya kwanza (first draft) ya katiba yetu na kikao kijacho waje nayo. Ila waliambiwa ni vyema tarehe 15/ 10/2011 rasimu ya kwanza iwe tayari.

KUONGEZA NGUVU YA JUMUIYA
Baadhi ya wajumbe walikiambia kikao kuwa waliwahi kusikia kuwa kuna wenzetu wa Arusha Sekondari nao wana umoja wao hapa Dar. Hivyo ikapendekezwa kuwa ni bora tuwatafute na tuwashirikishe katika shughuli za Jumuiya yetu. Hivyo basi tuliwaomba Kaka Tumaini Kimathi na Peter Mgasa waweze kuwatafuta.